Psychology

KWANINI NA LINI UNAPASWA KUMUONA MWANASAIKOLOJIA?

Mawazo na tafsiri ya watu wengi ni kuwa anayepaswa kumuona mwanasaikolojia au mnasihi (Counselor) ni mtu alipungukiwa na akili, wendawazimu au vichaa. Tafsiri hii sio sahihi kabisa na ni tafsiri iliyojaa unyanyapaa ndani yake.

☆☆☆☆☆ 0.0 (0 reviews)
0 enrolled
all
Swahili
Nicodem Patris Tingai
Nicodem Patris Tingai
Counselling Psychologist

Share this course

KWANINI NA LINI UNAPASWA KUMUONA MWANASAIKOLOJIA?
Free
Register to Enroll
  • Secure online access
  • Full lifetime access
  • Mobile & desktop
  • Certificate of completion

About This Course

Mawazo na tafsiri ya watu wengi ni kuwa anayepaswa kumuona mwanasaikolojia au mnasihi (Counselor) ni mtu alipungukiwa na akili, wendawazimu au vichaa. Tafsiri hii sio sahihi kabisa na ni tafsiri iliyojaa unyanyapaa ndani yake.
Wengine husema ‘kwanini nikamuone mbona haya mambo ni ya kwaida sana na kila mtu anayapitia’. Sio kweli, hakuna kilicho cha kawaidia katika maisha ya mtu, ndio maana tunatofautiana katika kufanya maamuzi, katika kukabiliana na changamoto. Hali hii inajidhihirisha hasa kwa kutokea matukio kama mauaji, kujidhuru na kuzuru wengine pamoja na uraibu wa aina mbali mbali.

Tiba ya kisaikolojia au Unasihi (Counselling) ni nini?
Kwa lugha rahisi kabisa, ni tiba ya mazungumzo ya kitaalamu baina ya mtaalamu na mteja. Mazungumzo haya hulenga kugundua na kutatua changamoto za kihisia na kiakili ambazo hazikusababishwa na madhara ya matibabu ya maradhi au matumizi ya dawa za aina yeyote. Huhusika Zaidi na hali ya kihisia na kiakili (emotional and mental state) kwa maana ya utatuzi wa changamoto za mfumo wa fikra na maamuzi (thinking patterns and decision-making processes).
Hivyo changamoto kama;
Kujihisi kuchoka na kazi sana na kushindwa kuendelea (burn-out)
Msongo wa mawazo,
Kushindwa kufanyaa maamuzi kwa mambo makubwa na muhimu,
Kuhimili hisia zinazo umiza sana, Mfano; kuvunjika kwa mahusiano na msiba
Namna bora ya kuanzisha mahusiano na kukaa katika mhusiano

Hii inamaanisha kwamba, kama vile mwili unavyochoka na kuumwa, akili na hisia pia huchoka. Huduma ya ushauri wa kisaikolojia ni kama "check-up" ya mfumo wako wa fikra na maamuzi.

Kwanini unamuhitaji Mwanasaikolojia/Mnasihi?
Labda ulikuwa hufahamu hili, Mwanasaikolojia au Mnasihi (Counselor) si rafiki tu wa kupiga naye stori bali pia ni mtaalamu anayekusaidia kuhimili mkandamizo wa kihisia na kimaamuzi unaoupitia. Ni msiri wako katika yale usiyoweza kuyaeleza kwa wengine. Kwa sababu ana uwezo wa kukusaidia kufikia malengo yako na pia anajua na anpaswa kulinda siri zako kisheria pia.
Tunamuitaji sana Msaikolojia /Mnasihi ili tuweze kupata msaada katika
Kujitambua: Kuelewa kwanini unajisikia au kutenda unavyotenda ambayo hukuwahi kufikiria au kutenda kabla.
Kujua chanzo/sababu na namna ya kutatua changamoto hizo: Msaikolojia/Mnasihi anakusaidia kuweza Kupata mbinu za kitaalamu za kuvuka magumu au changamoto unayopitia katika hali ya usalama Zaidi na namna gani ya kujikinga isitokee tena. Hali kama msongo wa mawazo, huzuni, au migogoro.
Sehemu Salama: Ni uhakika kuwa utapata mahali ambapo huwezi kuhukumiwa wala kulaumiwa na siri zako zinalindwa 100%, hakuna namna zinaweza kutolewa.

Lini/Wakati gani unapaswa kuchukua hatua?
Usisubiri mpaka mambo yaharibike kabisa. Ikiwa unajiona kwenye hali hizi, ni wakati wa kumuona mtaalamu:
Mabadiliko ya kihisia: Hasira za haraka, huzuni iliyokithiri, au kukosa furaha kwenye vitu ulivyokuwa unavipenda.
Kushindwa kupata Usingizi na kukosa hamu ya kula: hii huambatana na kulala sana au kukosa usingizi kabisa, na kupoteza hamu ya kula au kula kupita kiasi.
Kupata mawazo mabaya: Kushindwa kuzuia mawazo mabaya au hofu kuhusu mambo yajayo.
Kujitenga: Kutaka kuwa peke yako muda wote na kuepuka marafiki au wanafamilia.
Matumizi ya Vileo kupita kiasi: Kuanza kutumia pombe au dawa za kulevya kama njia ya "kusahau" matatizo.
Unapoona dalili hizi na Zaidi ambazo sio za kawaida katika mwili wako, katika tabia zako na mazingira yako, usichelewe, usifikirie sana, unamuitaji sana mnasihi kuweza kusaidiana naye kutatua changamoto hii.

Unahitaji nini kabla ya kumuona Mnasihi?
Kila jambo lina hatua zake, na hivyo unapoitaji kumuona mnasihi wako kuna hatua za kujiandaa ambazo zitakusaidia kupata matokeo yaliyo bora Zaidi; baadhi ya mambo hayo ni kama yafuatayo;
Jiulize, kwanini ninaitaji kumuona msaikolojia?
Je, nikionana naye ni unategemea juu ya changamoto yako?
Baada ya hapo, Kuwa Tayari kufunguka na kueleza ukweli kuhusu hali. Jua kuwa utahitaji kusema ukweli kuhusu hisia zako au changamoto yako kadri mnasihi atakavyokuongoza. Tambua kuwa Mnasihi hawezi kukusaidia usiposema ukweli.
Unaweza kuandaa au kuandika maswali madogo kuhusu unachopitia ili usisahau ukiwa mbele ya mnasihi na ukamweleza au kumuuliza.



Sasa unapaswa kufanya nini ili upate matokeo mazuri?
Unapoamua kuanza safari hii na kutafuta huduma ya kisaikolojia na unasihi, zingatia yafuatayo:
Chagua mtaalamu sahihi, hii ni muhimu sana. Hakikisha ni mtaalamu aliyesajiliwa na mwenye sifa.
Kuwa na uvumilivu, jua kuwa tiba na mabadiliko ya kisaikolojia hayaji kwa siku moja. Ni mchakato unaohitaji muda, ustahimilivu, uvumilivu na uaminifu kila hatua.
Kuonyesha Ushirikiano kwani Mnasihi ni muongoza njia tu, kazi kubwa ya kubadilika ipo mikononi mwako. Fuata muongozo na mazoezi au ushauri unaopewa kwa uaminifu.
Kuna na uaminifu kwa nafsi yako, Usifiche hisia kwa kuogopa kuonekana mdhaifu. Udhaifu wako ndio mlango wa kupona kwako.

Tamabua kuwa;
Kutafuta msaada wa kisaikolojia ni ishara ya nguvu, si udhaifu. Ni ujasiri wa kutaka kuwa bora kwa ajili yako na wale unaowapenda. Akili yako ndio injini ya maisha yako itunze!

Karibu nikuhudumie
About the Instructor
Nicodem Patris Tingai
Counselling Psychologist

Mimi ni Mwanasaikolojia Mnasihi (Counselling Psychologist), Mwanzilishi na Msimamizi wa Mindfree Psychology, nikiwa na uzoefu mpana wa kutoa huduma za Afya ya Akili kwa weledi, Usiri, na uhakika. Nimebobea katika kutoa ushauri na huduma za kisaikolojia kwa ujumla kama mahusiano, malezi kwa watoto na

Instructor
View Full Profile